Powered By Blogger

Monday 8 February 2010

JIKINGE


Kumbe twaweza. pakiwa na nia na kusaidiana .
Najua kila mtu anaweza kutoa mchango wake juu ya kupambana na Ukimwi.Tumezoea tu , tunapotaja Ukimwi kwanza tunafikiri pesa kwamba labda inahitaji mabilioni ya shilingi kupambana na ugonjwa huu tena yatoke kwa wafadhili ambao nao wamekubwa na mtikisiko kama si tetemeko la uchumi
Ndio tunaweza kupambana nao kwa kutumia pia rasilimali tulizonazo. Hivi mzee nyumbani kama atakaa na watoto wake na kuwafundisha maadili mema si amechangia kupambana na Ukimwi . Pia kwa wanandoa kama watakaa pamoja na kufundishana maadili ya ndoa kwa kuwa waaminifu katika ndoa zao ili siku moja virusi vya Ukimwi visijipenyeze katika familia vipi si watakua wamepambana na Ukimwi .
Basi mkabala wa waraka huu utajikita zaidi ni kwa jinsi gani tunaweza kupambana na ugonjwa wa Ukimwi kwa kutafuta suluhisho ambazo ziko ndani ya uwezo wetu

No comments:

Post a Comment