Wednesday, 10 February 2010

Wangar Maathai, Lulu ya AfrikaBi Wangari Maathai
Unaweza kuanza kitu kama utani tu lakini kikawa na mafanikio makubwa sana dunia . Tunakumbuka kuanzishwa kampuni kama microsoft ama TOYOTA ambayo ilikua kama karakana ya familia tu.Leo hii ni makampuni makubwa sana duniani yanayiongiza mabilioni ya shilingi kila mwaka .

Basi ndio hivyo ilivyoanza taasisi ya Wanaharakati wa Mapinduzi ya Kijani huko Kenya ama , Green Belt Movement . Hivi leo kweli utaamini kwamba asasi hiyo iliyoanzishwa na mwanamama jasiri wa huko Kenya . Bi Wangari Maathai , imebeba umaarufu mkubwa sana duniani na hata kufungua ofisi nje ya Kenya kama vile nchi za Ulaya .

Hebu angalia viunganishi vya makala hii fupi uone jinsi mwanamazingiza huyu alivyopania kuleta mabadiliko

Ukiangalia wasifu wa mama huyu bila shaka utakubali kwamba ni mmoja kati ya wanamama shupavu si Afrika tu bali dunia nzima . Amechangia kwa kiasi kikubwa masuala ya kuendleza shughuli za mazingira duniani akiwa mwana falsafa katika tasnia hiyo . Wasifu wake unaeleza kwamba pamoja na kushika nyadhifa mbalimbali huko nchini Kenya pia amefanya juhudi kubwa kiasi cha kutunukiwa tunzo sisizopungua 15 za kimataifa

No comments:

Post a Comment